The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

KIKAO CHA USHIRIKIANO WA VITEN...

KIKAO CHA USHIRIKIANO WA VITENGO VYA UFATILIAJI NA TATHMINI BAINA YA SEKTA YA MAJI NA NISHATI

Leo kimefanyika kikao cha ushirikiano wa vitengo vya ufatiliaji na tathmini vya wizara ya maji na wizara ya nishati, kikao icho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya maji Mtumba, Jijini Dodoma.

Katika kikao icho kilichoongozwa na mkurugenzi wa ufatiliaji na tathmini wa wizara ya nishati Bi. Anitha Tshengoma pamoja na mkurugenzi wa ufatiliaji na tathmini wa wizara ya maji Bi. Diana Kimario, wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika kufatilia na kutathmini miradi mbalimbali katika sekta ya maji na nishati ili kuendelea kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa.

“Ni muhimu kwa vitengo vya ufatiliaji na tathmini kuhakikisha sera na mipango ya wizara na taasisi zake inatekelezwa ipasavo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za maji na nishati kwa wananchi.”Amesema Bi. Anitha Tshengoma.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi wa ufatiliaji na tathmini wa wizara ya nishati amesema “Wizara ya maji na nishati tumekua tunafanya kazi kwa ukaribu zaidi kwa mda mrefu, ukizingatia wizara hizi zipo pamoja kwenye miradi ya kimkakati kama ule wa bwawa la mwalimu Nyerere na Kidunda" amesema Bi. Kimario

Pia Mchumi kutoka wizara ya maji Alex Kikalugai, amekiambia kikao icho kua kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji nchini imefikia asilimia 92.5 kwa maeneo ya mijini na asilimia 85.2 kwa maeneo ya vijijini

Katika kikao icho pia kimeudhuriwa na watendaji mbalimbali kutoka katika vitengo hivyo vya ufatiliaji na tathmini kutoka katika wizara zote mbili za maji na nishati.

Kikao icho pia kimeadhimia kuendelea kushirikiana ili kuendelea kuimarisha upatikanaji wa maji na nishati nchini